Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema serikali imefanikiwa kupunguza biashara ya uvuvi haramu kwa asilimia 80 kwa upande wa maji baridi na asilimia 100 kwa matumizi ya vilipuzi katika ukanda wa Bahari ya Hindi.
Amesema operesheni mbalimbali zilizofanywa na wizara kudhibiti uvuvi haramu, zimesaidia kupata ongezeko kubwa la mazao ya uvuvi.
Waziri Ndaki amesema, “mwaka 2020 jumla ya tani 497,567 za samaki zenye thamani ya Sh trilioni 2.34 zilivunwa ikilinganishwa na tani 362,645 zenye thamani ya Sh trilioni 1.48 mwaka 2015/2016.
Ameeleza kuwa kati yake, tani 435,408.9 ni kutoka maji baridi na tani 62,158.38 zilitoka maji chumvi ikilinganishwa na tani 409,332.72 zilizovunwa maji baridi na 60,976.51 kutoka maji chumvi kwa mwaka 2019.
Amesema ongezeko hilo ni kutokana na kupungua kwa uvuvi haramu.
Amesema uagizaji wa samaki kutoka nje ya nchi umepungua kwa 99.7% kutoka tani 22,962 zenye thamani ya Sh bilioni 56.12 mwaka 2016/2017 hadi tani 8.21 zenye thamani ya Sh bilioni 0.16 mwaka 2020