Home BIASHARAUWEKEZAJI Benki ya Dunia yawekeza dola 370m sekta binafsi

Benki ya Dunia yawekeza dola 370m sekta binafsi

0 comment 119 views

Benki ya Dunia (WB) inayotoa mikopo na misaada kwa sekta binafsi (IFC), imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 370 kwa ajili ya kuendeleza sekta hiyo nchini.

Akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano na Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameishukuru WB na kusema

“Sekta binafsi ni injini ya ukuaji uchumi hivyo uwekezaji mkubwa wa rasilimali fedha unahitajika ili sekta hiyo iweze kuchochea shughuli za uzalishaji na maendeleo ikiwemo kilimo na mifugo, nishati, na maeneo mengine mtambuka ili kuleta tija katika sekta hizo na hatimaye kuchangia katika pato la Taifa.”

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, ameeleza kuwa Zanzibar inahitaji kuwa na sekta binafsi imara kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia wa IFC Sergio Pimenta, ameahidi kwamba Taasisi yake inatarajia kuongeza kiwango cha uwekezaji wa mitaji kwa sekta binafsi nchini Tanzania hivi karibuni.

Mafanikio haya ni matokeo ya mkutano kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mtendaji wa IFC, Makhtar Diop, wakati wa ziara yake aliyoifanya nchini Tanzania mwezi Februari 2022, ambapo alimwomba Kiongozi huyo kuisadia sekta binafsi ili iweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa

Utekelezaji wa mipango hiyo ya kuiwezesha sekta binafsi utasaidia kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wenye thamani za shilingi trilion 114.8 ambao umeainisha kuwa asilimia 40 ya utekelezaji wa mpango huo sawa na shilingi trilioni 40.6 zinatakiwa kutoka katika sekta binafsi huku asilimia 60 ya gharama za mpango huo sawa na shilingi trilioni 74.2 zinatakiwa kutoka Serikalini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter