Home BIASHARAUWEKEZAJI China, Tanzania kukuza soko mazao ya bahari

China, Tanzania kukuza soko mazao ya bahari

0 comment 112 views

Ushirikiano baina ya Tanzania na China unawezesha utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa buluu na utalii ambao unahusisha usafirishaji wa mazao ya Bahari ikiwemo samaki.

Waziri wa Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Shaban Omary amesema hayo Julai 4, 2023 katika hafla ya siku ya China (CHINA DAY) katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) katika viwanja vya Mwl. J.K.Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha amewashauri Watanzania kufika katika maonesho hayo ya 47 ili kujionea na kutumia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya nchi na zile zilizopo nchini China.

Waziri Shaban ameeleza kuwa kutokana na ushirikiano huo baadhi ya makampuni kutoka China yameanza kutengeneza vyumba ya kuhifadhia bidhaa (COLD ROOM) ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya bahari ikiwemo samaki na kukuza uchumi wa bluu.
Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesena China ni washirika wakubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa eneo la biashara la Ubungo litakalo kuwa na Malls nyingi.

Naye Balozi wa Jamhuri ya China Chen Mingjian amesema maadhimisho hayo yameendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kitamaduni kati ya
Tanzania, China na Africa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter