Home BIASHARAUWEKEZAJI Dola 167 milioni kuwekezwa Pwani

Dola 167 milioni kuwekezwa Pwani

0 comment 128 views

Kampuni 13 kutoka China zimefanya maamuzi ya kufanya uwekezaji utakaogharimu Dola za Marekani milioni 167 ambazo ni sawa na bilioni 384.1 za kitanzania katika sekta ya viwanda mkoa wa Pwani katika eneo la uwekezaji la Kiluwa. Wawekezaji hao wameonyesha nia ya kuwekeza katika viwanda kutengeneza treni, betri za magari na cha usindikaji. Mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo ametoa shukrani zake kwa Mkurugenzi Mtendaji wa eneo la uwekezaji la Kiluwa Free Processing Zone, Mohammed Kiluwa kwa kuwaleta wawekezaji hao nchini.

Mkuu huyo wa mkoa amesema wawekezaji hao wana teknolojia za kisasa na fedha za kuwekezea hivyo hakuna haja ya kuwanyima fursa hiyo ya kuwekeza, ambapo ndani ya wiki moja au mbili zijazo wawekezaji hao watakuwa wamepewa mrejesho kuhusu namna ya kuipata ardhi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe, amesema ni jukumu la kituo hicho kutafuta wawekezaji lakini wananchi pia wanaruhusiwa kuwaleta wawekezaji kama ambavyo Kiluwa amefanya. Pia ameongeza kuwa hadi sasa kampuni 6 kati ya 13 tayari zimeshaingiza mashine zao nchini .

Kwa upande wake, Mohammed Kiluwa ameshukuru uongozi wa mkoa huo kwa kushiriki katika kutekeleza azma ya Rais Magufuli ya kufikia ya uchumi wa viwanda na kuomba serikali kuharakisha taratibu za kuwapa ardhi wawekezaji hao kufuatia ushindani uliopo na nchi nyingine.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter