Home BIASHARA ARCA yafanyika kwa mara ya kwanza Tanzania

ARCA yafanyika kwa mara ya kwanza Tanzania

0 comment 40 views
Na Mwandishi wetu

Kongamano la sita la Utafiti barani Afrika (ARCA) limefanyika kwa mara ya  kwanza hapa nchini kwa kushirikiana na  Chuo cha Biashara (CBE), Wakala wa Vipimo (WMA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa CBE limeanza jana tarehe 17 Agosti na linatarajia kumalizika kesho tarehe 19 Agosti.

Akiongea katika uzinduzi wa kongamano hilo ambalo limefanyika nchini kwa mara ya kwanza, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde amesema ni fursa ya Tanzania kushirikiana na nchi mbalimbali ili kuongeza wigo katika uchumi wa viwanda nchini katika awamu hii ambayo Tanzania inapanga kujiimarisha kiuchumi.

Mavunde amesema kuwa serikali imewekeza fedha za kutosha vyuoni ili kufanikisha kufanya utafiti na nchi mbalimbali ili kukuza uchumi wa viwanda na kuweza kutoa huduma na bidhaa bora hapa nchini kwani kuwepo kwa ongezeko la viwanda kutasaidia changamoto ya ajira kwa vijana na kuongeza pato la taifa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TBS Prof. Egid Mubofu amesema kuwa nchi yetu inajivunia kukidhi vigezo vya TBS na vigezo vyote duniani, huku Mkuu wa Chuo cha CBE Prof. Emanuel Mjema amesema ili kuwa na mahusiano mazuri na nchi mbalimbali ni lazima kuwepo na vigezo vya kupima viwango bora ili kujua takwimu sahihi ya watu wanaopata huduma.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter