
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Madini, Mh. Doto Biteko (wa pili kushoto)
Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati
alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini
Geita.Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said
Kalidushi (kulia).

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita iliyoandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNDP) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.