Home BIASHARAUWEKEZAJI JPM: Wizi wa madini udhibitiwe

JPM: Wizi wa madini udhibitiwe

0 comment 167 views

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amemtaka Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko kuanzisha vituo vya madini katika maeneo mbalimbali nchini yanayozalisha migodi. Rais Magufuli amesema hayo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha viongozi wapya wa serikali na kueleza kuwa maagizo hayo yanalenga kudhibiti madini yanayoibwa na kupelekwa nje ya nchi na kupelekea nchi kushindwa kunufaika ipasavyo na maliasili zake.

“Ripoti mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki zinaonyesha Tanzania kuwa nyuma katika uuzaji wa dhahabu wakati sisi ndio tunaongoza katika uchimbaji, kwa ripoti hii ni lazima tujiulize tunakwama wapi? Dhahabu tunazochimba zinauzwa wapi? Soko lipo wapi na tunalijua? Tunapouza tunapata fedha kiasi gani? Wizara ipo na wataalamu wake na hapo ndio changamoto inapoonekana” Alisema Rais Magufuli.

Pamoja na maagizo hayo, Rais Magufuli pia ameagiza Waziri Biteko kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuweka mkakati utakaowezesha nchi kuanza kununua dhahabu na kuitunza. 

“Tanzania lazima isimame, hatuwezi kuendelea kuibiwa dhahabu, lazima tutunze dhahabu yetu, itatufaa hata Shilingi yetu ikishuka”. Amesisitiza Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter