Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda amesema nusu ya mapato yanayotokana na kivutio cha Olduvai Gorge wilayani Ngorongoro, yataelekezwa katika makumbusho ya taifa ili kuhakikisha makumbusho hayo yanayohifadhi mabaki ya kihistoria na kiakiolojia yapo katika hali nzuri ambayo itaendelea kuwavutia watalii wanaofika nchini kutembelea.
Katibu huyo amesema makumbusho nyingi nchini hazina mandhari ya kuridhisha, jambo ambalo sio sawa na hivyo hatua zinatakiwa kuchukuliwa ili kufanya mabadiliko. Profesa Mkenda ametaja moja ya makumbusho hayo kuwa makumbusho ya taifa ya Dar es Salaam ambayo haina vifaa vya kisasa vya kuhifadhia mabaki ya kihistoria kama mifupa.
Tanzania inategemea kuwakilishwa na watayarishaji wa rekodi 150 hadi 180 katika tamasha la biashara litakalofanyika Machi 6-10 mwaka huu nchini Ujerumani na hivyo kuwavutia watu zaidi ya 10,000 kutoka dunia nzima.
Olduvai Gorge ambayo ipo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Uhifadhi Ngorongoro (NCAA) imetajwa kua moja ya vyanzo vikuu vya mapato katika sekta ya utalii. Kwa mwaka 2016/2017 Shilingi bilioni 1.9 zilizalishwa katika kivutio hicho ambacho kinatumia nyenzo za kisasa tangu mwaka 2017.