Home BIASHARAUWEKEZAJI Qatar, Tanzania kushirikiana

Qatar, Tanzania kushirikiana

0 comment 61 views

Rais John Pombe Magufuli na Naibu Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Shehe Mohammed bin Abdulrahman J.A. Al Thani wamefanya mazungumzo kuhusu masuala ya uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo mbili, Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa na ugeni huo na kumueleza Shehe Mohammed kuwa, Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji zikiwemo uchakataji wa gesi, madini, utalii, na usafiri wa anga na kumuomba kiongozi huyo kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji nchini Qatar kuja kuwekeza Tanzania.

“Natambua Qatar mna utaalamu wa kuchakata gesi na sisi tunayo gesi nyingi, kwa hiyo nawakaribisha mje tushirikiane kuwekeza katika sekta ya gesi. Na pia natambua kuwa nyie ni wanunuzi wakubwa wa dhahabu, sisi tunayo dhahabu nyingi na hivi sasa tumeanzisha vituo vya ununuzi wa dhahabu, nawakaribisha mje mnunue dhahabu na tutawapa ushirikiano wote mtaouhitaji. Amesema Rais.

Mbali na kutuma salamu zake kwa Mtawala wa Qatar, Shehe Tamim bin Hamad Al Thani, Rais Magufuli ameiomba serikali ya nchi hiyo kuendelea kushirikiana na Tanzania hasa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama uzalishaji wa umeme, ujenzi wa reli, barabara na madaraja.

Kwa upande wake, Shehe Mohammed amemshukuru Rais Magufuli na serikali yake na kueleza kuwa Qatar ipo tayari kufanyia kazi maombi aliyowasilisha Rais Magufuli na kwamba nchi hizo zitaendelea kushirikiana.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter