Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais wa Ujerumani kuzungumza na vijana Watanzania

Rais wa Ujerumani kuzungumza na vijana Watanzania

0 comment 215 views

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier atafanya ziara ya kikazi nchini Tanzania kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 01 2023.

Ziara hiyo imelenga kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji pamoja na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inasema ujumbe wa Rais Steinmeier utajumuisha viongozi wengine wa serikali pamoja na wawekezajiwa makampuni makubwa 12.

“Akiwa nchini, Rais Steinmeier atafanya mazungumzo na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Oktoba 31, 2023 na baada ya mazungumzo hayo viongozi hao watapata fursa ya kuongea na wandishi wa habari kueleza kuhusu masuala muhimu yaliyofikiwa katika mazungumzo yao,” imesema taarifa hiyo.

Maraisi hao pia watapata fursa ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara litakalokutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wan chi hizo mbili lililoandaliwa na ubalozi wa Ujerumani kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Aidha, Rais Steinmeier anatarajiwa kuonana na kuzungumza na vijana wajisiriamali wa Kitanzania wanaojihusisha na uvumbuzi wa teknolojia mpya mahususi ya akili bandia (AI) ambap wanafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Novemba 01, 2023 Rais Stenmeier atasafiri kwenda Wilayani Songea mkoani Ruvuma kutembelea Makumbusho ya vita vya Maji Maji na shule ya msingi Majimaji.

“Hii ni makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonyesha historia kubwa ya vita vya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani,” inasema taarifa hiyo.

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 60.

Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati hususani biashara na uwekezaji, maji, afya, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake, uhifadhi wa bioanuai, usimamizi wa fedha, utalii pamoja na malikale na utamaduni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter