Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali ya Tanzania yawekeza bilioni 25.7 utafiti, ubunifu na maendeleo ya teknolojia

Serikali ya Tanzania yawekeza bilioni 25.7 utafiti, ubunifu na maendeleo ya teknolojia

0 comments 54 views

Katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali kupitia Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imewekeza sh bilioni 25.7, kwa ajili ya kufanya utafiti, ubunifu na maendeleo ya teknolojia katika maeneo mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu jijini Dodoma Machi 17, 2025, wakati akitaja mafanikio ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan toka aingie madarakani.

Amesema hatua hii si tu kwamba imeendelea kuimarisha msingi wa maendeleo ya kisayansi, bali pia imethibitisha dhamira ya Serikali ya kujenga taifa linalowekeza katika kuibua teknolojia, likiongozwa na tafiti na ubunifu.

Dkt. Nungu amesema Serikali kupitia COSTECH, imefadhili zaidi ya tafiti 50 katika sekta za Elimu, kilimo, afya, na mazingira ili kuhakikisha maarifa haya yanatumika kuboresha maisha ya Watanzania.

Amesema zaidi ya vituo vya ubunifu 111 vimeimarishwa, huku tafiti zikibadilika kuwa suluhisho kisayansi kwa jamii, zikiwemo kampuni mpya zipatazo 70 zimesajiliwa yote hayo yakiwa na matokea ya wabunifu waliyowezeshwa na Serikali.
Ame

sema kupitia mfumo wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Serikali ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na taasisi za kimataifa, COSTECH imepokea shilingi bilioni 5.65 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya utafiti wa pamoja kati ya watafiti wa Tanzania na washirika wetu.

Vilevile kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Serikali imetenga shilingi bilioni 6.3 kwa ajili ya miradi ya utafiti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, huku shilingi milioni 600 zikielekezwa katika miradi minne ya usalama wa chakula, ikihusisha udhibiti wa magonjwa ya mazao, uboreshaji wa uhifadhi wa chakula na ubunifu wa vyakula vyenye virutubishi vya hali ya juu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!