Home BIASHARAUWEKEZAJI Tabora yashauriwa kuwa na dawati la uwekezaji

Tabora yashauriwa kuwa na dawati la uwekezaji

0 comment 104 views

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla aneshauri kuanzishwa kwa dawati maalum litakalokuwa na taarifa zote muhimu za uwekezaji mkoani Tabora ili kuwasaidia wale walio na malengo ya kuwekeza kuchagua kwa usahihi kulingana na vipaumbele vyao. Makalla amesema kuwa moja kati ya jukumu la dawati hilo ni kuonyesha fursa za kipekee zilizopo mkoani huo ambazo zinaweza kuwavutia wawekezaji kuwekeza kwenye hoteli, viwanda na ufugaji wa kisasa.

Makalla ametoa wito huo mkoani Tabora ambapo alikaribishwa kushiriki na kufungua mkutano wa maandalizi ya Jukwaa la Biashara na Uwekezaji likatalofanyika mwezi ujao. Mkuu huyo wa mkoa amefafanua kuwa hatua hiyo inapaswa kwenda sanjari na wilaya zote mkoani humo kuorodhesha maeneo yanayofaa kwa uwekezaji na vilevile kuangalia uwezekano wa kuyapima.

“Kwa mfano mnaweza kusema kwa sababu Sikonge wana misitu mingi hapa panafaa kujenga kiwanda cha kusindika na kuchakata asali, Igunga wanazalisha pamba kwa wingi kijengwe kiwanda cha kuchambua pamba na nyuzi zake, Nzega kuna ng’ombe kijengwe kiwanda cha ngozi na kusindika nyama, Urambo wanalima sana tumbaku kijengwe kiwanda cha tumbaku na Kaliua kijengwe kiwanda cha unga”. Ameshauri Makalla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter