Home BIASHARAUWEKEZAJI TIC yampongeza JPM, yamfurahia Angellah Kairuki

TIC yampongeza JPM, yamfurahia Angellah Kairuki

0 comment 249 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe amesema kituo hicho kimefurahishwa na hatua ya Rais wa Tanzania Dk. John  Magufuli kuanzisha Wizara inayojikita na masuala ya uwekezaji kwani hapo awali, shughuli zote za kituo hicho zilikuwa chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Mwambe amesema TIC imefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli kumteua Angellah Kairuki kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji na kusema kufanya hivyo kutachangia kutelekeza majukumu ya masuala ya uwekezaji ipasavyo.

Mwambe amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, umuhimu wa kituo hicho katika kujenga uchumi wa nchi kupitia sekta ya uwekezaji ni mkubwa huku akisisitiza kuwa, uwepo wa viongozi ni chachu ya nchi kuelekea uchumi wa kati kupitia uwekezaji katika viwanda.

“Jana niliongea Waziri wa Fedha na Mipango, alitusisitiza tujitahidi sana kujenga mazingira ya uwekezaji na yawe rafiki zaidi asiwepo mtu wa kukwepa kulipa kodi na tukifanya hivyo tutamsaidia sana Rais na wawekezaji waendelee kuiona Tanzania kuwa nchi salama katika uwekezaji”. Amesema Mwambe.

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa taasisi binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali, kushiriki kikamilifu katika kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter