Home BIASHARA Mauzo ya Tanzania Ujerumani Dola 42.05m kwa mwaka

Mauzo ya Tanzania Ujerumani Dola 42.05m kwa mwaka

0 comment 57 views

Tanzania imekuwa ikiuza nchini Ujerumani bidhaa zenye thamani ya wastani wa Dola za Marekani milioni 42.04 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Mmamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bidhaa kuu ambazo Tanzania inauza Ujerumani ni pamoja na kahawa, asali, tumbaku, pamba, samaki, nta na vito vya thamani.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaeleza kuwa Tanzania pia inaagiza bidhaa kutoka Ujerumani zenye wastani wa Dola za Kimarekani milioni 237.43 kwa mwaka.

Bidhaa hizo ni pamoja na dawa, vifaa tiba, mafuta (manukato na vipodozi) magari, vifaa na mashine za umeme.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kwa upande wa uwekezaji, Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini.

“Kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121,” imesema taarifa hiyo.

Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imefanikiwa kusajili miradi 15 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300.00 ambayo imezalisha ajira 905.

Kampuni za Kijerumani zilizowekeza nchini zinajihusisha zaidi na sekta za kilimo, viwanda, nishati mbadala, ujenzi, utalii, sanaa na utamaduni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter