Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji wanaonyanyasa wananchi waonywa

Wawekezaji wanaonyanyasa wananchi waonywa

0 comment 96 views

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu amewataka wawekezaji wenye tabia ya kuwanyanyasa wananchi kwa kuwakataza kuingia katika maeneo yao kwa ajili ya kupata huduma za kijamii kuacha tabia hiyo mara moja kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea migogoro ndani ya jamii.

“Ni kweli kuna wawekezaji ambao wana maeneo makubwa wananyoyamiliki kihalali na wanalipia kodi serikalini, lakini wamekuwa wakiwazuia wananchi kuingia katika mashamba yao hata kuokota kuni wakati kuna mabaki ya miti iliyokauka na kuoza”. Amesema Kitundu.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza kuwa baadhi ya wawekezaji wamekuwa wakizuia wananchi katika mashamba yao licha ya kwamba hayajaendelezwa, na wananchi hao wanahitaji huduma ya maji na kuchunga mifugo yao pasipo kufanya vurugu au uharibifu.

Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa wawekezaji wengi, hasa wanaotoka nchi za nje wamekuwa hawatoi ushirikiano kwao na kudai kuwa ni wamiliki halali wa ardhi hiyo kwa mujibu wa Sheria. Wametoa wito kwa wawekezaji hao kuishi vizuri na jamii inayowazunguka kwani wakiendelea kuwanyanyasa wananchi, hali ya vurugu inaweza kujitokeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter