Home BIASHARA Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Dodoma

Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Dodoma

0 comment 124 views

Kampuni ya simu za mkononi Vodacom imeunga mkono juhudi za serikali kuhamia mji mkuu wa Dodoma kwa kufungua makao yake makuu kanda ya kati.

Juhudi hizo zimefanywa kuhakikisha wateja wa Vodacom wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge, akikata utepe kuzindua ofisi mpya za kanda ya kati na duka la kisasa la Vodacom Tanzania Plc jijini Dodoma. Kampuni hiyo imezindua makao yake makuu ya Kanda ya Kati ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu. Wa pili kulia ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Kati wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bi Grace Chambua. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya za Kanda ya kati na duka la kisasa la Vodacom Tanzania Plc jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.

Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter