Home VIWANDAMIUNDOMBINU SRG awamu ya kwanza kukamilika mwakani

SRG awamu ya kwanza kukamilika mwakani

0 comment 102 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema sehemu ya kwanza ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka jijini Dar es salaam hadi Morogoro inatarajiwa kukamilika Novemba 2019, huku ile inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Dodoma ikitarajiwa kumalizika Februari 2021. Ujenzi huo ambao kwa pamoja unakadiriwa kugharimu Sh. 7.1 trilioni, fedha ambazo ni kodi za watanzania unafanywa kwa vipande vipande ili ukamilike kwa wakati.

 

“Kila kipande kinasimamiwa na meneja wake na tunafanya hivi ili twende na wakati kwani kila kipande kitajengwa bila kuathiri kipande kingine”. Ameeleza Mkurugenzi huyo.

 

Hadi kufika sasa, ujenzi wa SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro umekamilika kwa zaidi ya asilimia 34 na takribani madaraja 26 yanatarajiwa kujengwa ili kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huo.

 

“Zaidi ya yote ujenzi huu umetoa ajira 6,500 kwa watu mbalimbali kama madereva, wahandisi na mafundi”. Amesema Kadogosa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter