Home BIASHARA Vodacom Tanzania wazindua kituo cha kutoa huduma Makambako

Vodacom Tanzania wazindua kituo cha kutoa huduma Makambako

0 comment 280 views

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom Tanzania imezidi kusogeza huduma zake karibu kwa wateja wake kwa kufungua kituo kipya cha kutoa huduma jijini Makambako, Njombe.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Makambako Bw Paul Malala aliyesifu ukuaji wa Vodacom na kuhimiza wazidi kuongeza vituo vya kutoa huduma katika jiji hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Makambako Bw Paul Malala, akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo cha kutoa huduma cha Vodacom Tanzania jijini Makambako, Njombe jana. (Kushoto) ni Mteja wa Vodacom Emmanuel Gadau, Meneja Mauzo wa Njombe, Humphrey Mutabiirwa na Msimamizi wa Maduka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Yasinta Hussein. Vodacom Tanzania imelenga kuongeza upatikanaji wa huduma ili kuwezesha maendeleo ya jamii.

Msimamizi wa Duka, Mussa Ndazi, akielezea juu ya huduma mbali mbali zitakazo tolewa katikaa kituo kipya cha Vodacom Tanzania kilichozinduliwa jijini Makambako, Njombe jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Makambako Bw Paul Malala. Vodacom Tanzania imelenga kusogeza huduma zake ili kuwezesha maendeleo ya jamii.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter