Home BIASHARA Hatujazuia Fastjet kuingiza ndege-TCAA

Hatujazuia Fastjet kuingiza ndege-TCAA

0 comment 140 views

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari amesema mamlaka hiyo haijazuia Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania kuleta ndege zake tarehe 22 Desemba mwaka huu kama Shirika hilo lilivyopanga na kufafanua kuwa kilichotokea ni maombi ya kuwasilisha ndege yaliwasilishwa Desemba 24. Johari amewaambia waandishi wa habari kuwa tangu kupewa notisi, Fastjet imewasilisha andiko tarehe 24 Desemba na mpaka sasa TCAA inalifanyia kazi.

“Madeni ya Fastjet yalikuwa zaidi ya Sh. 6 bilioni ambazo wanadaiwa na watu tofauti, tayari wamelipa sehemu ya fedha wanazodaiwa na TCAA japo si zote. Usafiri wa ndege una masharti ya msingi ambayo yasipofuatwa ni hatari. Miongoni mwa mambo ya msingi ni uwezo wa kifedha katika Shirika, usafiri wa anga hakuna ujanja kama hatakidhi masharti leseni itafutwa tukisema tuhurumiane ni hatari tutaua watu, usafiri wa anga usiposimamiwa vizuri ni hatari kwa usalama utaua watu”. Ameeleza Mkurugenzi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter