Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imetumia mfumo mpya wa alama za vidole kusajili wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Vodacom imewezesha wafanyakazi wake na vifaa hiyvo vya kusajili ili kuwaezesha kufikisha huduma karibu na wateja wake.

Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Michael Mhando na Emmanuel Medukenya wakisajili wanafunzi kwa kutumia mfumo mpya wa alama za vidole katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma, jijini humo. Hivi karibuni kampuni hiyo imewezesha wafanyakazi wake na vifaa vya kusajilia kwa kutumia alama za vidole ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wateja wake popote nchini.