Home BIASHARA Vodacom wazindua simu janja kuwasaidia wateja kuingia ulimwengu wa kidigitali

Vodacom wazindua simu janja kuwasaidia wateja kuingia ulimwengu wa kidigitali

0 comment 88 views

Vodacom Tanzania Plc, kampuni nambari moja ya mawasiliano ya simu nchini imeungana na kampuni ya TECNO kuwaletea wateja wao toleo jipya la simu aina mbili za TECNO Yente na Itel Bamba, leo jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni harakati ya Vodacom kuhakikisha jitihada zake za kuwezesha maisha ya kidijitali kwa wateja wao, kwa kupitia simu janja zinafanikiwa.

Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa simu hizo, Mkuu wa matukio wa kampuni ya TECNO, Anuj Khosla alisema, “Tumedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa la Tanzania kuwa la kidijitali”.

Simu hizi zitapatikana kwa bei ya shilingi 75,000 kwa Itel Bamba- 3G na Shilingi 195,000 kwa TECNO Yente ambayo ni – 4G, simu zote mbili zinakuja na ofa, ambapo kwa simu ya Itel Bamba wateja wetu watapata GB 3 kila mwezi kwa miezi minne na kwa simu ya TECNO Yente watapata GB 2 kila mwezi kwa mwaka mzima.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania Plc, Nandi Mwiyombella akionyesha simu mpya aina ya TECNO Yente iliyozinduliwa kwa ushirikiano kati ya Vodacom na TECNO katika hafla fupi iliyofanyika Duka la Vodacom Mlimani City Dar es Salaam, jana. Kampuni ya Vodacom imewaletea wateja wao simu hizo kwa lengo la kuwawezesha kuwa na maisha ya kidijitali kupitia simu janja bora zinazouzwa kwa bei nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Matukio wa Kampuni ya TECNO, Anuj Khosla.

“Tunafuraha kushirikiana na TECNO kuendelea kuimarisha zaidi azimio letu la kuzidi kuwawezesha wateja wetu kuwa katika ulimwengu wa kidijitali. Uzinduzi huu umekuja katika kipindi muafaka, hasa kwakuwa Watanzania wengi zaidi wanatumia huduma za simu janja” alisema Nandi Mwiyombella, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.

Katika zama hizi za kidijitali, kupata taarifa, kununua na kulipia vitu, na kupata burudani za muziki na sinema, vinawezekana kwa kutumia simu janja, na matoleo haya mapya ya TECNO Yente na ITEL Bambayatawezesha hayo yote na zaidi. “Uzinduzi huu umekuja sambamba na msimu wa sikukuu ya nanenane ili kuhakikisha wateja wetu, ambao ndiyo kipaumbele chetu wanasherehekea sikukuu ya nanenane msimu huu kidijitali zaidi” aliongeza Bi. Mwiyombella.

Simu hizi zitapatikana katika maduka yote ya Vodacom Tanzania Plc  na pia katika madawati ya huduma kwa mteja (Service Desks) yanayotoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo maeneo mbalimbali nchini huku pia zikipatikana katika maduka ya TECNO.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter