Home BIASHARA Vodacom yadhamini mkutano wa 39 wa SADC

Vodacom yadhamini mkutano wa 39 wa SADC

0 comment 128 views

Katika kuhakikisha wageni mbalimbali kutoka nchi jirani wanapata mawasiliano kwa urahisi, kampuni ya simu ya Vodacom imedhamini mkutano wa SADC na kuweka kituo ambapo wageni waalikwa wa mkutano huo wanaweza kusajili lain za Vodacom.

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya akisikiliza huduma mbali mbali zitolewazo na kampuni ya Vodacom Tanzania kutoka kwa Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Alex Bitekeye, katika banda lao kwenye mkutano wa 39 wa SADC , jijini Dar es salaam, hivi karibuni. Katika mkutano huo kampuni ya Vodacom Tanzania imedhamini upande wa mawasiliano ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika.

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya akisoma ripoti ya uwekezaji katika maendeleo ya watu na mpango mpya ya Vodacom Tanzania Foundation, aliyenaye ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Alex Bitekeye, katika banda lao kwenye mkutano wa 39 wa SADC , jijini Dar es salaam, hivi karibuni. Katika mkutano huo kampuni ya Vodacom Tanzania imedhamini upande wa mawasiliano ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter