Kampuni ya simu za mkononi Vodacom imeibuka na tuzo katika maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika mwanzoni wa mwezi wa nane. Vodacom imeshinda tuzo ya kampuni bora kwa upande wa mawasiliano kanda ya kaskazini.
Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Mh. Abdallah Ulega alikabidhi tuzo hiyo kwa Mkuu wa mauzo wa kanda ya Kaskazini, Bi. Brigita Stephen akishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo.
Vodacom inaendelea kuboresha huduma zake kwa kuziweka kidijitali ili kwenda sambasamba na mwenendo wa ulimwengu.

Mtaalamu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Mandela Seth, akiwapa maelezo ya kutumia kifaa cha intaneti (modem) wateja waliotembelea banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.

Wakazi wa Bariadi mkoani Simiyu wakipatiwa huduma mbalimbali kwenye banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.