Katika kuhakikisha inafikisha mawasiliano nchi nzima kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom imezindua kituo kipya cha kutoa huduma kwa wateja mjini Tunduma. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Bw. Juma Ilando ambae aliwashukuru Vodacom na kuwaomba kuzidi kuongeza vituo vya kutoa huduma kwa wateja wilayani hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Bw. Juma Ilando akikata keki baada ya kuzindua duka la Vodacom Tanzania wilayani hapo ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuwafikia wateja wake. Kulia kwake ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya nyanda za juu Kusini, Bw. MacFadyne Minja (mwenye shati nyeusi) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tunduma.

Wanamuziki wakiburudisha katika uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania mjini Tunduma, ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuwasogezea wateja wake huduma.