Home BIASHARA Wafanyabiashara Sido wauza nje ya soko

Wafanyabiashara Sido wauza nje ya soko

0 comment 141 views

 

Na Mwandishi wetu

Wafanyabiashara katika soko la Sido jijini Mbeya ambalo liliteketea kwa moto usiku wa kuamkia Agosti 15 wameamua kufanya biashara zao nje ya soko hilo wakati wanasubiri vibali vya kuanza ujenzi wa vibanda vya kudumu. Wafanyabiashara hayo wamedai kuwa wamefikia hatua hiyo ili waendelee kujiingizia kipato kipindi hiki ambacho bado wanasubiri maelekezo kutoka kwa viongozi.

Uongozi wa serikali ya mkoa wa Mbeya umewaruhusu wafanyabiashara hao kuendelea na ujenzi wa vibanda vya kudumu kwa sharti la kufuata michoro maalum ambayo imeandaliwa na wataalamu. Hivi sasa baadhi ya wafanyabiashara wamepanga biashara zao nje ya soko hilo huku wengine wakiuza kwenye magari yao.

Moto uliotokea katika soko hilo umekadiriwa kuleta hasara ya takribani Sh.14.29 bilioni huku tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto huo ikitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni jiko la mkaa lililokuwa katika moja ya mabanda sokoni hapo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter