Home BIASHARA Wafanyabiashara wa mbao, karafuu kuunganishwa India

Wafanyabiashara wa mbao, karafuu kuunganishwa India

0 comment 75 views

Wafanyabiashara wa mbao, karafuu na mazao ya mikunde nchini wameunganishwa na soko la India ili kuuza bidhaa hizo.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu kikao baina ya Nayan Patel ambae ni Mwakiishi wa Heshima wa Tanzania Mumbai- India na wafanyabiashara hao.

Taarifa ya TanTrade inasema kwa lengo la kikao hicho ni kuwaunganisha wazalishaji nchini na soko la India.

Akizungumza katika kikao hicho, Patel ameeleza kuwa India ina uhitaji mkubwa wa mbao (teak na pine), karafuu, pilipili manga, mbaazi, dengu na parachichi.

Amesema ametembelea Tanzania kwa lengo la kuwaaunganisha wauzaji na wasambazaji wa bidhaa hizo na wanunuzi kutoka India.

‘’Nilianzia biashara nchini Ujerumani ambapo nilitengeneza daraja la kuunganisha biashara kati ya makampuni makubwa ya India na Ujerumani na sasa nipo tayari kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na India ili kufanya biashara ya mazao haya kwa pamoja na kujipatia masoko na kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.

Pia nipo tayari kuwasaidia wafanyabiashara kutoka Tanzania wanaoagiza bidhaa kutoka India,’’ amesema.

Patel ameeleza kuwa India ina fursa kubwa katika viwanda vya ufungashaji na viwanda vya dawa ambapo kuna zaidi ya viwanda 500 vinavyotengeneza vifungashio.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa M. Khamis, Afisa Biashara Mkuu kutoka TanTrade Freddy amesema Tanzania ina mahusiano mazuri na India na kwa upande wa biashara inauza bidhaa za kilimo, madini na mazao ya misitu.

Aidha Tanzania huagiza madawa, mashine, vipuri, vifaa vya ujenzi kutoka India.

Amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha mahusiano ya kibiashara na India ili kuongeza zaidi mauzo ya bidhaa zetu katika soko la India.

Jumla ya wafanyabiashara ishirini na sita (26) wameshiriki kikao hicho na kuishukuru TanTrade kwa kuwaletea karibu fursa za masoko kutoka nchi mbalimbali na kuahidi kuchangamkia kutumia fursa hizo kwa manufaa ya biashara zao na Taifa kwa Ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter