Home VIWANDA Dodoma mpya ya viwanda yasifiwa

Dodoma mpya ya viwanda yasifiwa

0 comment 47 views

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema viwanda mkoani humo vimefanikiwa kuongezeka hadi kufikia 2,347 mwaka huu kutoka 1,716 mwaka 2015, ikiwa ni ongezeko la asilimia 37. Dk. Mahenge amesema kuongezeka kwa viwanda kumepelekea mafanikio mbalimbali na kueleza kuwa, takribani viwanda 2,308 ni vidogo huku 25 vikiwa vya kati na nane vikiwa viwanda vikubwa. Viwanda hivyo vimekadiriwa kutengeneza ajira 23,470 za kudumu.

Mkuu huyo wa mkoa pia amedai mkoa huo umetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo la kila mkoa kuanzisha viwanda 100 ambapo mkoa wa Dodoma umefikia lengo hilo na kuna jumla ya viwanda vipya 115 na hadi sasa, 62 kati ya hivyo vimekamilika na vimeanza shughuli za uzalishaji.

“Viwanda 52 vipo katika hatua za ujenzi na tunatarajia vitakamilika kabla ya Desemba 2018”. Amesema Dk. Binilith.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter