Home BIASHARA Wanunuzi samaki walizwa na ushuru

Wanunuzi samaki walizwa na ushuru

0 comment 157 views

Imedaiwa kuwa samaki aina ya sangara hutozwa ushuru wa Sh. 200 kwa kilo moja katika Halmashauri ya Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanunuzi wa Sangara, Gregory Kazimbo, amesema kuwa wanunuzi wa samaki hao wanalalamikia tozo ya ushuru ya Sh. 200 kwa sababu inawalazimu kununua Shilingi 3,500 kwenye mialo na kuuza katika viwanda kwa Shilingi 4,000 ambayo hailipi.

“Tumepeleka maombi yetu katika Halmashauri hiyo ili Baraza la Madiwani litusaidie kubadilisha ushuru huo mkubwa kwa kila kilo ya samaki Sh. 200. Tunaomba iwe angalau Shilingi 30″. Amesema Kazimbo.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa awali, Halmashauri ilikuwa ikiwatoza ushuru wa jumla ambao ulikuwa Sh. 100,000 kwa tripu lakini baadae wakabadilisha mfumo huo na kuanza kuwatoza Sh. 200 kwa kilo, jambo ambalo linakwamisha sana biashara zao hivyo kuwataka wabadilishe mfumo huo na kuwatoza angalau 150,000 kwa tripu.

Kazimbo amesema mabadiliko ya tozo hizo yatawasaidia kukabiliana na majukumu ya kila siku kwani hivi sasa, wanapata shida kutokana na kupata faida ndogo. Mwenyekiti huyo ametaja baadhi ya majukumu hayo kuwa ni michango ya kijamii, malipo ya kodi TRA, malipo Sumatra, ushuru wa viwanda na leseni za ukusanyaji samaki na usafirishaji na mengine mengi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter