Home BIASHARA Waziri Mhagama: Mabaraza ya biashara yafanye kazi

Waziri Mhagama: Mabaraza ya biashara yafanye kazi

0 comment 102 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu) Jenista Mhagama amesema uwepo wa Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya (RBC’s/DBC’s) utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa vikwazo vinavyorudhisha nyuma harakati za biashara na uwekezaji. Akizungumza akiwa ziarani kukagua miradi inayoratibiwa kwa ubia baina ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na Taasisi ya Kuboresha Mazingira ya Biashara Mikoani (LIC), Waziri huyo ameitaka TNBC kuhakikisha mabaraza yote mikoani yanafanya kazi.

“Mabaraza ya mikoa na yale ya wilaya yapo katika nafasi nzuri sana kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa shughuli za biashara na uwekezaji kuimarika na hatimaye kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa. Ninapenda kuona mabaraza katika mikoa yote yanakuwa hai kwa kuwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa urasimu na vikwazo visivyo vya muhimu na kuchangia kuimarika kwa biashara hapa nchini”. Amesema Waziri Mhagama.

Mbali na hayo, Waziri huyo pia amesisitiza kuwa serikali imedhamiria kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kuvuta wawekezaji na kupitia TNBC, amesema jambo hilo litawezekana.

“Serikali inajitahidi kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuvutia wawekezaji wa ndani na wale wa nje ili iweze kukusanya kodi ambayo ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote duniani”. Amesema Waziri Mhagama.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter