Home Elimu Benki ya Equity yazindua mkopo kufadhili elimu nje ya nchi

Benki ya Equity yazindua mkopo kufadhili elimu nje ya nchi

0 comment 22 views

Benki ya Equity imezindua mkopo mpya wa elimu uliobuniwa mahsusi kwa ajili ya wazazi wa Kitanzania wanaoishi nchini ambao wanataka kufadhili elimu ya watoto wao nje ya nchi.

Tukio hili liliendeshwa na timu ya Benki hiyo ikiongozwa na Haidar – Mkuu wa Kitengo Cha Malipo, na Eric – Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Diaspora, sambamba na wazazi mbalimbali walioshiriki kwa dhati katika majadiliano kuhusu jinsi suluhisho hili linavyoweza kubadilisha fursa za kielimu za watoto wao.

Taarifa ya benki hiyo inaeleza kuwa mkopo huo unagharamia ada za masomo na gharama za maisha kwa ngazi za diploma, shahada ya kwanza, uzamili, na uzamivu, ukiwa na masharti nafuu ya marejesho na riba shindani inayokidhi mahitaji ya wateja wetu.

“Mkopo huu si tu unawawezesha familia kufanikisha malengo yao ya kielimu, bali pia unachangia ukuaji wa uchumi wa taifa kwa kukuza nguvu kazi yenye ujuzi na ushindani wa kimataifa. Suluhisho hili linaendana na dira ya serikali ya kuongeza fedha zinazotumwa kutoka nje hadi kufikia dola za Mrekani 1.5 bilioni ifikapo mwaka 2028.

Benki ya Equity inaendelea kujidhatiti kuwawezesha familia za Kitanzania kwa kutoa suluhisho za kifedha zilizobuniwa mahususi kufungua fursa za maendeleo na ustawi wa kijamii,” imesema taarifa hiyo.

Tukio hilo lilifanyika katika Serena Hotel, Dar es Salaam, likiwaleta pamoja wateja wa diaspora, wadau, na wazazi wa Kitanzania kujadili mahitaji yao ya kifedha na kuzindua suluhisho mpya za kifedha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter