Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimezindua programu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu ili kuweza kukidhi vigezo katika soko la ajira kwa kushirikiana na Taasisi ya Gen Empower ambapo Rais mstaafu ambae pia ni Mkuu wa chuo hicho, Dkt. Jakaya Kikwete alisema ana imani itakuwa chanzo cha kuondoa na kumaliza kabisa tatizo la ajira nchini.
“Isiwe fahari kwa wanafunzi kukaa vyuoni kwa miaka mitatu au zaidi na kuishia kuvaa majoho na kurejea majumbani,” amesema Dkt. Kikwete katika uzinduzi programu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu ili kuweza kukidhi vigezo katika soko la ajira.
Programu hiyo ya miaka mitano, imelenga kuwaongezea vijana ujuzi na maarifa ili kuweza kupata ajira na kujiari wenyewe badala ya kusubiria ajira.