Muungano wa Afrika (AU) umeipitisha lugha ya Kiswahili, kuwa lugha rasmi ya kikazi ndani ya Umoja huo.
Kiswahili pia kimeridhiwa kuwa lugha ya saba kutambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) duniani.
Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kirusi , Kiarabu na Kispanyola ni lugha nyingine zinazotambulika dunia.
Consolata Mushi ni Kaimu Katibu wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetangaza kuwa Kiswahili kimetengewasiku maalumu ambayo itakuwa ni ya maadhimisho ya Kiswahili, Julai 7 kila mwaka.
“Hatua hii ni muhimu na inafanya Kishwahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutengewa siku maalumu ya kutambuliwa na UN,” amesema.
Kiswahili ni miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa na atu wengi dunia. Kwa sasa kina wazungumzaji zaidi ya nmilioni 200 duniani, kinafundishwa katika vyuo vikuu zaidi ya 58 duniani.