Home Elimu UDSM yatakiwa kuangalia ubora wa wanafunzi katika soko la ajira

UDSM yatakiwa kuangalia ubora wa wanafunzi katika soko la ajira

0 comment 108 views

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

UDSM imetakiwa kuangalia ubora wa wanafunzi wanaowatengeneza katika soko la ajira.

Katika miaka 60 ya UDSM, ambapo pia kulikuwa na maadhimisho ya miaka 57 ya Ndaki ya Sayansi ya Jamii (College of Social Science CoSS) mada mbalimbali zilijadiliwa ambapo vijana wengi walionekana kutokidhi matakwa ya soko la ajira.

Amina Lumuli, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Shirika la Reli Tanzania ameeleza kuwa wahitimu wengi wanashindwa kujieleza wakati wa usaili wa kutafuta ajira.

“Unashangaa mtu amemaliza chuo, wakati unamfanyia usaili analia na hawezi kujieleza, hata kuandika sentensi mbili wengine wanashindwa,” ameeleza Amina.

Amekitaka chuo hicho kuangalia ubora wa wanafunzi wanaozalisha ili waweze kushindana katika soko la ajira Afrika na dunia kwa ujumla.

Mkuu wa Ndaki ya Sayansi ya Jamii Profesa Christine Noe amesema wanaangalia jinsi ya kuboresha mfumo wa ufundishaji na mitaala ili wahitimu waweze kuendana na soko la ajira lililopo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon maarufu kama NickwaPilli ambae alikuwa mmoja wa wazungumzaji amesema ni vyema wakufunzi waweke mazingira rafiki ya ufundishaji na kozi zinazovutia wanafunzi kusoma.

“Kunatakiwa kuwe na ubunifu, ufikiri wa kina katika kuandaa wahitimu pamoja na kuangalia ubora kuliko wingi wa wahitimi,” amesema Simon.

Mzungumzaji mwingine Daktari Elia Emmanuel amesisitiza katika ufundishaji unaokwenda na wakati (sayansi na teknolojia).

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu inayosema “Miaka 60 ya Umahiri wa Sayansi ya Jamii katika Taaluma, Utafiti na Huduma za Jamii.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter