Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania imeshiriki kwenye maonyesho ya Techfest yalioandaliwa na kampuni ya Robotech yanayolenga kuinua vijana kwenye fani ya teknolojia.
Kampuni ya Vodacom kupitia mpango wake wa instant schools inaendelea kuinua na kuhimiza vijana kujiingiza kwenye fani ya teknolojia ili kutanua uelewa wao na kupanua fursa zao za kupata ajira kwenye masoko ya dunia.

Mkurugenzi Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akitazama bunifu mbali mbali zilizofanywa na wanafunzi katika maonyesho ya Techfest yaliyoandaliwa na kampuni ya Robotech kwa ajili ya kuinua vijana kwenye fani ya teknolojia, jijini Dar es Salaam, wikiendi hii. Kampuni ya vodacom Kupitia mpango wake wa Instant schools inaendelea kuinua na kuhimiza vijana kujiingiza katika fani ya technologia ili kutanua uelewa wao na kupanua fursa zao kupata ajira kwenye masoko ya dunia. Alieambatana naye ni muandaaji wa maonyesho hayo Shaukatal Zahir.