Taasisi ya Vodacom Foundation imetoa mchango wa madawati 300 yenye thamani ya TZS milioni 61 kwa wanafunzi 400 katika shule ya msingi ya Salunda na Somanda wilayani Bariadi.
Taasisi hiyo imetoa mchango huo kusaidia jitihada za serikali katika kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini.

Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Salunda na Somanda wakiwa wamekalia madawati yaliyokabidhiwa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, jana wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Taasisi hiyo imetoa madawati 300 yenye thamani ya TZS milioni 61 kwa shule hizo ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia serikali kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini.