Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom imeandaa tamasha la ‘Bring your kid to work’ ambalo lilifanyika makao makuu ya ofisi hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika Tamasha hilo watoto walishirki michezo mbalimbali na pia kujionea jinsi wazazi wao wakifanya kazi.
Vodacom imekua kampuni ya kwanza Tanzania kuandaa tamasha la namna hii.

Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc wakifurahia michezo mbali mbali katika tamasha la “Bring your Kid to work” lililofanyika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Kampuni ya Vodacom ni ya kwanza nchini kuandaa tamasha la namna hiyo ambapo watoto wamepata nafasi kuona jinsi wazazi wao wanavyotekeleza majukumu yao ofisini hapo.

Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc wakifundishwa jinsi ya kutumia platform ya instant School ambayo inawawezesha wanafunzi kupata vitabu vya masomo mbali mbali, katika tamasha la “Bring your Kid to work” lililofanyika makao makuu ya ofisi za Vodacom mwishoni mwa wiki.