Home Elimu Wahitimu kidato cha nne 2024 wapewa siku 30 kubadili tahasusi

Wahitimu kidato cha nne 2024 wapewa siku 30 kubadili tahasusi

0 comments 16 views

Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imetoa fursa ya siku 30 kwa Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2024 kubadili tahasusi zao (combination) au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalamu stahiki katika maisha yao ya baadaye ambapo utaratibu huo umeanza March 31 hadi April 30 mwaka huu.

Akiongea Jijini Dodoma April 02,2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema hatua hiyo inatoa fursa kwa Wanafunzi kubadilisha machaguo ya tahasusi za kidato cha tano na Vyuo vya Kati na Elimu ya Ufundi kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na Vyuo.

“Hatua hii ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha tano na Vyuo vya Serikali kwa mwaka 2025, Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa kidato cha nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combination) na Kozi mbalimbali walizozichagua kupitia Fomu ya Uchaguzi (Selform.)”

Amesisitiza kuwa “napenda kuwasihi wazazi na walezi kushauriana kikamilifu na watoto wao na kupata ushauri wa kitaalamu na kabla ya kufanya machaguo sahihi ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao”.

Mchengerwa amewahimiza wahitimu wote kufanya marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi unaopatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz ambapo mhitimu anapaswa kuandika jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama za ufaulu alioupata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.

“Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za kidato cha tano na kozi mbalimbali katika vyuo vya Kati na elimu ya ufundi, kwa kuzingatia ufaulu na chaguzi zao”amesema Waziri Mchengerwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!