Home Elimu Wanafunzi watakiwa kuchangamkia Scholarship

Wanafunzi watakiwa kuchangamkia Scholarship

0 comment 148 views

Wito umetolewa kwa vijana na wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari kuchangamkia fursa za udhamini wa masomo wa hadi asilimia 50 (Scholarship) zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala nchini Tanzania (Kampala International University in Tanzania (KIUT) ).

Katika maonyesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Tecknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, Mkufunzi wa KIUT Martin Nyolobi amesema udhamini huo unalenga kuwasaidia vijana wanaosoma masomo ya sanaa (arts) na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo.

“Vyuo vingi hususani vya serikali vimekuwa vikitoa kipaumbele kwa kuwapa ufadhili wa masomo wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi, sisi sasa tumeona tutoe ufadhili huu kwa wanafunzi wa masomo ya arts ambao wanaonekana kusahaulika.” Amesema Nyolobi.

Amefafanua kuwa “kwa mwanafunzi atakayejiunga na KIUT kwa muhula wa masomo 2021/2022 atapata udhamini wa masomo mpaka 50% kwa masomo yasiyo ya Afya kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada.”

Amesema ni wakati muafaka sasa kwa wanafunzi kuchangamkia fursa hiyo kwa kufanya usaili kabla Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) haijafunga usaili kwa mwaka huu mapema mwezi ujao.

Ili kupata udhamini huo, mwanafunzi ni lazima afanye maombi ili waweze kusajiliwa kupata (admissions letter) ambayo itaambatanishwa na barua ya kuomba udhamini katika ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) alipotoka.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter