Home Elimu Wananchi watakiwa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa

Wananchi watakiwa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa

0 comment 7 views

Wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia Taasisi za Fedha zilizosajiliwa ambazo zinazingatia Sheria, kanuni na taratibu katika huduma za fedha ili kujiepesha na watoa huduma za fedha wasio sajiliwa.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha,  Dadi Kolimba, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha waliofika wilayani hapo kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Fedha, ili kuwawezesha wananchi kuwa na uelewa wa masuala ya fedha.

Kolimba amesema kumekuwa na baadhi ya taasisi zinazotoa mikopo kwa wananchi ambayo haifuati Sheria hivyo kusababisha malalamiko ya mara kwa mara na kusababisha wananchi kupoteza mali zao ambazo wameweka dhamana.

Wananchi wa Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha wakisikiliza mafunzo ya maswala ya fedha.

‘‘Tulishazungumza na watoa huduma za fedha na taasisi za fedha hapa wilayani na tukasisitiza kuwa mikopo wanayotoa isiwaumize wananchi na endapo tukigundua wanaenda kinyume na Sheria tutawachukulia hatua za kisheria na tunasisitiza

Akizungumza kuhusu elimu inayoenda kutolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha wilayani humo, alisema kuwa elimu hiyo itasaidia wananchi kupata uelewa wa haki na wajibu wa mtoa huduma katika utoaji wa mikopo ili kuwasaidia kuondokana na mikopo umiza.

Kolimba ameeleza  kuwa ana imani elimu itakayotolewa kwa wananchi itawaongezea uelewa zaidi wa kutambua haki zao ikiwemo kufahamu taratibu za mikopo ikiwemo kiasi cha riba watakachotozwa na taasisi ya fedha katika mikopo wanayochukua kabla ya kuchukua mkopo.

‘Natoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo haya ya kutoa elimu kwa wananchi na pia nimpongeze Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo haya kuhakikisha kuwa elimu hii ya fedha inawafikia wananchi ili kuondokana na changamoto za kiuchumi‘’, ameongeza Kolimba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter