Home Fashion Tanzania nchi ya kwanza Afrika mwenyeji Mashindano ya Urembo Dunia

Tanzania nchi ya kwanza Afrika mwenyeji Mashindano ya Urembo Dunia

0 comment 111 views

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika na ya 12 duniani kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 28, 2022 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas amesema shindano hilo litafanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Ameeleza kuwa katika shindano hilo, Rais Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Doroth Gwajima Waziri wa Jinsia, Wanawake na Makundi maalum huku Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa atakuwa mgeni maalum.

Amesema tukio hilo litarushwa na mitandao mbalimbali duniani pamoja na kituo cha televisheni cha AZAM ambacho kitarusha mbashara kupitia kipindi chake cha Sinema zetu kuanzia majira ya saa mbili usiku.

Pia amesema katika tukio hili   maalum itawajumuisha waalikwa zaidi ya 1000.

amesema filamu ya Royal Tour itaanza kuonyeshwa ili watu waweze kuona jinsi Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii.

Aidha, ameongeza kuwa burudani kutoka kwa wasanii wa muziki mbalimbali zitaoneshwa na ameomba washiriki kuwa tayari kupokea matokeo kutoka kwa majaji.

Dkt. Abbas ameeleza kuwa serikali imewapa zawadi washindi wote wa shindano hilo la kidunia na viongozi kutembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro Oktoba 31,2022 baada ya kumalizika kwa shindano hilo ikiwa ni mwendelezo wa Royal Tour aliyoiasisi Rais Samia.

Hilo litakuwa ni shindano la 12 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter