Home FEDHA Bilioni 200 kwa ajili ya machinga

Bilioni 200 kwa ajili ya machinga

0 comment 135 views

Benki ya NMB imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwapa mikopo wamachinga.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi amesema wameingia mkataba na wamachinga ambapo mbali na mikopo hiyo, benki hiyo pia itawapa mafunzo ya kifedha.

“Kupitia ujuzi tulionao tutakuwa tukitoa mafunzo kwa machinga, benki yetu ina uzoefu mkubwa na tumekuwa tukiwapa mafunzo wajasiriamali kupitia NMB business Club.

Ni wajibu wetu kuhakikisha tunainua wafanyabiashara wadogo ‘Machinga’ kiuchumi,” amesema.

Mikopo hiyo itatolewa kuanzia kiasi cha shilingi laki tano hadi milioni tano.

Kwa upande wa umoja wa wafanyabiashara ndogondogo (machinga) wamesema fedha hizo siyo tu zinakwenda kuwasaidia kwenye mitaji yao, bali zinawavusha kutoka kwenye umasikini na kuwa matajiri.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter