Home FEDHABIMA Benkiwakala inaleta ushindani huduma za bima: Mwigulu

Benkiwakala inaleta ushindani huduma za bima: Mwigulu

0 comment 151 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Mfumo wa Benkiwakala wa Bima umesaidia kukuza biashara ya Bima nchini.
Dk Mwigulu ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini Innocent Edward Kalogeris aliyetaka kujua kama Serikali haioni kuwa kuruhusu Benki kuwa Wakala wa Bima, Mawakala wengine watafunga biashara kwa kukosa wateja.
Dk. Nchemba amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na wadau wa bima ilianzisha Benkiwakala wa Bima ili kuongeza wigo wa usambazaji na upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi.

“Idadi ya Wakala wa Bima wa Kawaida imekuwa ikiongezeka sambamba na Benkiwakala wa Bima kwa sababu hali hii imechochea ushindani, ubunifu na kutegemeana”, amebainisha Dk. Nchemba.

Amesema Takwimu zinaonesha Benkiwakala waliosajiliwa ni 14 kwa mwaka (2020), 23 (2021), 27 (2022) na 30 hadi Machi 2023.

Kwa upande wa Wakala wa Bima wa kawaida waliosajiliwa ni 745 kwa mwaka (2020), 789 (2021), 910 (2022) na 960 kati ya Julai 2022 na Machi 2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter