Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa la Tanzania (NIC) Sam Kamanga amesema shirika hilo linatarajia kuanzisha programu ya bima ya kilimo kwani zaidi ya asilimia 75 ya watanzania wanategemea kilimo kuendesha maisha yao.
Kamanga amesema hayo mkoani Pwani na kufafanua kuwa programu hiyo itaanza mwaka huu kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya sabasaba pamoja na siku ya wakulima maarufu kama nanenane. Kupitia bima hiyo, mkulima anaweza kulindwa endapo majanga mbalimbali yatatokea hali ambayo itampa unafuu na kusaidia kuepusha matumizi makubwa.