Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema jiji la Dodoma linaongoza kwa makusanyo ya mapato kwa mwaka 2017/2018 na limekusanya takribani Sh. 21 bilioni na kufanikiwa kuvuka lengo la kukusanya Sh. 20 bilioni.
Kunambi ameeleza hayo wakati akitoa takwimu kwenye ufunguzi wa maonyesho ya wajenzi Dodoma ambapo ametaja mikoa majiji mengine matano yanayoifuata Dodoma.
Amelitaja jiji la Dar es salaam kuwa na makusanyo ya ndani ya Sh. 18 bilioni, Arusha Sh. 14 bilioni, Mwanza Sh. 14 bilioni, Tanga Sh. 14 bilioni pamoja na Mbeya iliyofanikiwa kupata Sh. 11 bilioni.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, makusanyo yaliyopatikana pamoja na kigezo cha watu zaidi ya 500,000, ni sababu tosha ya halmashauri ya manispaa ya Dodoma kupandishwa hadhi na kuwa Jiji la Dodoma.