Na Mwandishi wetu
Siku chache baada ya Bodi ya Mikopo ya Elimu Ya Juu (HESLB) kutangaza masharti mapya kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na wale wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2017/2018, Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema ( BAWACHA) amesema Bodi ya mikopo inabagua wanafunzi na kuwakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Mojawapo ya masharti yaliyoongezwa na bodi hiyo ni pamoja na watoto wa wazazi viongozi au wanasiasa kutowepa mikopo kabisa jambo ambalo Mdee anasema ni ubaguzi kwani viongozi kama wadiwani hawana mishahara, lakini Bodi hii imetumia hoja nyepesi na zisizo na mantiki kuwanyima watoto wao mikopo.
Mdee amesema hoja itawasilishwa bungeni kupingana na masharti haya ambayo serikali imeyapitisha kwani kwamujibu wa katiba ya Tanzania kila mmoja na haki ya kupata elimu. Aliongeza kuwa serikali ilitakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata elimu na kupewa mikopo.