Home FEDHAHISA Wanahisa wa DSE wategemee gawio kubwa

Wanahisa wa DSE wategemee gawio kubwa

0 comment 147 views

Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) linatarajia kutangaza gawio kubwa kwa wanahisa wake kufuatia kufanya vizuri kwa kampuni hio baada ya kujiunga na kuuza hisa zake zenyewe kwenye soko hilo.

Wachambuzi wa masuala ya hisa wanasema DSE ipo katika nafasi nzuri kutangaza gawio kubwa kwa wanahisa wake kufuatia kufanya vizuri kimapato kwa miaka miwili sasa tangu ijiunge na soko.

Taarifa za fedha ya kampuni hiyo zimeonyesha kuwa ada ya kujiunga na soko inayotozwa kwa makampuni yanayotaka kujiunga imekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa DSE. Ada hiyo imechangia asilimia 41 ya mapato kuanzia Januari hadi Aprili 2018 and kuchangia wastani wa asilimia 36 kwa miaka miwili iliyopita.

Imeelezwa pia kuwa faida zitokanazo na uwekezaji ndio chanzo cha pili cha mapato kwa kampuni hiyo. DSE  ilitangaza faida ya asilimia 40 kwa miaka miwili na pia ilionyesha kuwa na fedha za kutosha za kujiendesha.

DSE inatarajia mwenendo mzuri wa biashara na hivvo kutangaza gawio kubwa kwa wanahisa wake. Gawio la mwisho lilitolewa oktoba mwaka jana na la nyuma lilikua Machi 2017 na Julai 2016 katika kipindi cha miezi tisa kwa kiasi cha Sh. 42 kwa hisa moja.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter