IMEANDIKWA NA ABHILASH GUPTA NA KUTAFSIRIWA NA LEAH NYINDIKE.
Wote tunapitia kipindi ambacho hatuna hela, hatuna malengo na matakwa huku tumefulia. Ikiwa tumefulia tunapaswa kuwajibika katika hali zetu kwa sababu sisi ndio tumesababisha.
Hakuna mtu ambaye atakujali zaidi kuliko wewe mwenyewe. Zifuatazo ni sababu za kwanini umeishiwa fedha na nini kifanyike ili kuondokana na hali hiyo.
1.Huamini katika bajeti
Bajeti ni mchakato wa kugawa kiasi flani cha fedha ambacho utatumia kwa ajili ya vitu mbalimbali kwa mwezi. Hii ni moja ya sababu kubwa kwanini umefulia. Hauamini katika bajeti, haujui mwelekeo wa matumizi yakona inawezekana haujui pesa yako inaenda wapi kila mwisho wa mwezi. Unaacha mshahara kulipa malipo yote.
Anza kufanya bajeti.
2.Unajilinganisha na watu wenye uwezo
Kulinganisha sio kuzuri sana hasa kama unafanya uwiano kwenye masuala ya fedha. Kufanya uwiano kunakufanya uwe na matarajio makubwa na utaumia endapo hujayafikia matarajio hayo. Maisha ni kama mbio na kila mtu ana mbio zake. Wengine wako mbele na wengine wako nyuma lakini wote wanakimbia kwenda muelekeo mmoja. Usilinganishe kipato chako na mali zako na watu matajiri. Anza kufanyia kazi malengo yako.
Jilinganishe wewe wa sasa na wewe wa zamani.
3.Huwezi kusema hapana
Kusema ndio kwenye kila kitu ni kuwa mwema, lakini si jambo jema kila muda. Jifunze kusema hapana. Mtoto wako akiwa analilia mdoli ukamnunulia, atalilia midoli mingine tena. Usisubiri tabia hiyo ikidhiri jifunze kusema hapana.
Ukiwa mwema kwa kila mtu kazini kwako, watachukua nafasi hiyo kumaliza kazi zao. Tafuta namna njema ya kusema hapana kwa vitu visivyo vya muhimu kwenye maisha.
4.Unalaumu serikali kwa matatizo yako
Kitu kisipoenda sawa unaishutumu serikali na kulalamika kuhusu matatizo yako. Ukilipa kodi zaidi, unalaumu serikali kwa kuongeza viwango vya kodi, ukiona kitu ni ghali, unatoa lawama kwa serikali na uchumi.
Acha kulaumu serikali kwasababu ya matatizo yako. Panga mipango kutokana na mabadiliko yanayokuzunguka.
5.Kulaumu badala ya kutafuta suluhisho
Sawa na kuilaumu serikali. Unawalaumu watu wengine mambo yako yasipoenda vile ulivyotarajia. Usilalamike kuhusu matatizo yako na kuwashtaki watu wengine. Tafuta njia ya kuyatatua matatizo yako badala ya kutoa lawama kwa watu.
6.Unapenda pesa
Moja ya sababu umefulia ni unapenda sana pesa. Uko makini sana na ‘balance’ ya akaunti yako na unaiangalia kila siku. Una mapenzi sana na pesa unaishia kuota kuhusu kupesa kuongezeka kwenye akaunti yako baadala ya kuchukua hatua itakayoongeza pesa.
Anza kuchukua hatua na usipende sana kuangalia kiasi kilichopo kwenye akaunti yako kila siku.
7.Umeacha kujifunza
Kujifunza ni mchakato wa maisha. Wale wanaoacha kujifunza huwa wanaacha kuishi. wanakuwa hawajui mambo mapya yanayotokea duniani hivyo kushindwa kuchanganua mawazo mapya. Mawazo mapya yanatusaidia kuchukua hatua ili kuyatekeleza. Hatua hupelekea matokeo mazuri. Tukiacha kujifunza tunakataa kufanya hatua.
Usiache kujifunza.
8.Una matumizi mabaya
Matumizi ya kupita kiasi ya vitu vibaya ni moja ya tabia mbaya. Uvutaji sigara, Pombe, madawa ya Kulevya, na matumizi ya kupindukia ya majukwaa ya kijamii zote hizi ni tabia mbaya ambazo zinaweza kuepukika. Unapoteza pesa na muda ukiwa unajihusisha na tabia mbaya hali itakayokupelekea kutokua na pesa. Unajiskia vibaya na huna furaha na maisha yako.
Acha matumizi mabaya ya fedha zako.
9.Huna malengo
Ni muhimu katika maisha yako kuwa na malengo. Bila malengo ya kueleweka utakuwa hujui nini unafanya katika maisha yako. Utaishia kulalamika kuwa unakosa muda wa kukamilisha shughuli zako kutokana na kutokuwa na malengo katika maisha.
Kuwa na malengo ya muda mfupi, na ya muda mrefu. Panga siku yako na kazi zako za kila siku. Taratibu utapata mrejesho mzuri wa mipango yako.
10.Unashinda na watu wasiokufaa
“Wewe ni wastani ya watu 4-5 unaoishi nao. Mara nyingi”
Chagua marafiki zako kwa busara. Tafuta watu wenye maslahi sawa na ushrikiane nao. Jaribu kuangalia kama mnaweza kutekeleza malengo yenu yanayofanana kufanya kazi kama timu kunakupa mawazo zaidi na malengo kutoka kwenye mitizamo tofauti.
Kwahiyo chagua watu wenye busara, ili kutimiza malengo yako.