Home FEDHA Mabilioni kukarabati Uwanja wa Ndege Songwe

Mabilioni kukarabati Uwanja wa Ndege Songwe

0 comment 152 views

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani humo unatarajia kufanyiwa ukarabati mkubwa unaokadiriwa kugharimu Sh. 18 bilioni. Chalamila amesema hayo wakati wa mapokezi ya ndege ya Airbus A220-300 ambayo imeanza safari zake za Dar es Salaam kwenda Mbeya

“Hatuna neno kuu kwa Rais, zaidi tunasema ‘asante na Mungu ambariki’, ndege hii imeleta neema kubwa hapa Mbeya, hivi karibuni uwanja huu utaanza kukarabatiwa,huo ni uamuzi wenye tija na upendo kwa Tanzania uliofanywa na Rais wetu, John Magufuli”. Amesema Chalamila.

Mbali na hayo, Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa hatua stahiki zitachukuliwa kwa baadhi ya watumishi waliohusika na upotevu wa mabilioni wakati wa ujenzi wa uwanja huo ambao amedai kiwango chake hakina ubora unaostahili.

Baadhi ya wakazi wa jijini humo wametoa wito kwa Rais Magufuli kuangalia njia mbadala itakayosaidia kupunguza gharama za usafiri wa anga ili kila mwananchi hususani aweze kuzimudu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter