Home BIASHARA TFDA yaimarisha huduma vituo vya forodha kulinda soko la ndani

TFDA yaimarisha huduma vituo vya forodha kulinda soko la ndani

0 comment 34 views

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kaskazini imesema itaendelea kulinda soko la ndani la bidhaa za vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa kuimarisha huduma katika mipaka yote nchini ikiwemo mpaka wa Namanga jijini Arusha ili kuhakikisha kuwa bidhaa bora na salama pekee ndio zinaingia nchini.

Hayo yameelezwa katika kituo cha TFDA kilichopo Namanga wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto pamoja na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo walipotembelea kituo hicho cha ukaguzi ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano.

Akizungumzia suala hilo, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kaskazini Benny John amesema ofisi hiyo imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo udhibiti wa vifaa tiba, chakula, dawa na vitendanishi kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata kanuni na Sheria zilizopo.

“Udhibiti wa bidhaa zinazoingia nchini umeongezeka kwa wafanyabiashara kulipa ada na tozo za serikali na hivyo kuongeza pato la taifa”. Ameeleza Kaimu Meneja huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter