Home FEDHA Majaliwa ashtukia ufisadi Kigoma

Majaliwa ashtukia ufisadi Kigoma

0 comment 108 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amegundua matumizi mabaya ya fedha za umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhingwe mkoani Kigoma na kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi. Majaliwa amemtaka Kamanda wa TAKUKURU mkoani humo Raphael Mbwambo kufuatilia ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo baada ya kuwa na wasiwasi na makadirio ya ujenzi huo. Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa halmashauri ya Buhigwe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wilaya unaofanyika Ruheta.

“Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kigoma fuatilia ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe na tunataka tujue ni nani aliyetengeneza makadirio hayo kwa sababu makadirio aliyofanya ni makubwa ukilinganisha na mradi husika”. Amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu ameagiza uongozi wa wilaya hiyo kupitia upya makadirio yaliyopo katika miradi mbalimbali ya ujenzi ili kuhakikisha ujenzi unaendana na makadirio yaliyowekwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter